NAIBU WAZIRI KATIMBA ATEMBELEA MABANDA YA MAONESHO, ACHOTA UZOEFU WA TAASISI ZA HAKI AFRIKA KUSINI
Tanzania kupitia ujumbe wa Wizara ya Katiba na Sheria ukiongozwa na Naibu Waziri Mhe. Zainab Katimba, umejifunza na kupata uzoefu utakaosaidia kuimarisha huduma za haki nchini pamoja na kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini katika sekta ya Sheria na Haki.
Uzoefu huu umepatikana kupitia ushiriki wa wizara katika Mkutano wa Kimataifa wa Upatikanaji wa Haki unaonendelea Sun City Afrika Kusini ambapo leo 13 Novemba, 2026 ni siku ya tatu ya Mkutano huo ulioanza tarehe 11 Novemba, 2023.
Mhe. Katimba ametembelea mabanda ya maonesho yaliyopo katika ukumbi wa mkutano, ambapo amepata fursa ya kujionea na kujifunza namna taasisi za haki za Afrika Kusini zinavyotekeleza majukumu yake na kuwahudumia wananchi.
Matembezi hayo yamempa Naibu Waziri na ujumbe wa Tanzania uzoefu wa vitendo utakaosaidia kuimarisha huduma za haki nchini Tanzania, sambamba na kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini katika sekta ya sheria na haki.