Dkt. Chana Apokea Cheti cha Heshima Kutoka Taasisi ya Kupinga Rushwa
Dkt. Chana Apokea Cheti cha Heshima Kutoka Taasisi ya Kupinga Rushwa
Imewekwa: 11 Dec, 2023

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amepokea cheti cha heshima kutoka Taasisi ya Kupinga Rushwa (Anti Corruptions Voices Foundations) alichotunukiwa kutokana na kuwa Mgeni Rasmi katika mbio za “Sepesha Rushwa Marathon.” Balozi Chana amekabidhiwa cheti hicho tarehe 10 Desemba, 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.