Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

KM Maswi Aikumbusha Tume ya Haki za Binadamu Wajibu Wake

Imewekwa: 05 Feb, 2025
KM Maswi Aikumbusha Tume ya Haki za Binadamu Wajibu Wake

Katibu Mkuu  Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi tarehe 5 Februali, 2025 Jijini Dodoma amefungua Baraza la 23 la Wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo Maswi amewasisitiza Watumishi na Viongozi wa  Tume hiyo kutumia Baraza hilo kukumbushana wajibu wao katika kuwatumikia Watanzani na kulinda misingi ya Haki na Utawala Bora.

“Ninategemea Baraza hili mlilokutana hapa mkitoka mtaleta mwelekeo mzuri wa utendaji kazi, naamini mnaelewa jukumu la Tume ni kusimamia, kuhifadhi na kulinda Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora” Amesema Maswi.

Baraza hilo litajadili mambo mbalimbali ikiwemo uwasilishaji wa utekelezaji wa shughuli za Tume hiyo kwa mwaka 2023/2024 na 2024/2025.