Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

MADEREVA WAMPA TUZO KATIBU MKUU MASWI KWA UTENDAJI BORA

Imewekwa: 11 Jul, 2025
MADEREVA WAMPA TUZO KATIBU MKUU MASWI KWA UTENDAJI BORA

Madereva wa Wizara ya Katiba na Sheria jana Julai 10, 2025 wamempa tuzo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakim Chacha Maswi kwa utendaji kazi wake ulio bora ambao umewezesha madereva hao kufanya kazi kwa ufanisi.

Madereva hao wamesema Katibu Mkuu Maswi ameboresha vitendea kazi pamoja na kuhakikisha Wizara ina magari ya kutosha, mavazi ya kitanashati kwa ajili ya kazi zao pamoja na kuwawezesha kupata chakula yaani mlo kamili wawapo kazini.

Naye Katibu Mkuu Maswi amewashukuru madereva hao na kuwakumbusha kuwa wao ni kiungo muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hivyo waendelee kufanya kazi kwa bidii, weledi na zaidi wayatunze magari kwani ndio ofisi zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Fatuma Kalovya amewataka madereva hao kuzingatia maelekezo ya kiongozi huyo huku akiwataka kuwa tayari kwa ajili ya mafunzo anuai yanayo wahusu madereva serikalini.