Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

MAHAKAMA ZANZIBAR KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA KESI KWA NJIA MBADALA

Imewekwa: 05 May, 2025
MAHAKAMA ZANZIBAR KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA KESI KWA NJIA MBADALA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamisi Ramadhani Abdalla amesema Mahakama ya Zanzibar imelenga kukazia njia mbadala ya utatuzi wa migogoro ikiwa ni pamoja na usuluhishi ili kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.

Jaji Khamisi ameyasema hayo leo wakati akizindua Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kusini Pemba leo tarehe 5 Mei 2025 katika uwanja wa Bustani ya Mwanamashungi Chake Chake.

Amesema kupitia usuluhishi wananchi wenye migogoro wataweza kuzungumza na kujadiliana ili kupunguza mrundikano wa kesi na gharama za kuendesha kesi mahakamani.

Jaji Khamis ameongeza kuwa katika mkoa wa Kusini Pemba Mahakama nne zinajengwa na katika Mahakama hizo kutakuwa na ofisi za Wasaidizi wa Kisheria ili wananchi wapate huduma kwa urahisi na kutatua migogoro kwa haraka

Ameeleza kuwa amewahi kufanya kazi katika mkoa wa Kusini Pemba na migogoro mingi aliyokutana nayo ni pamoja na masuala ya mirathi, ardhi, migogoro ya ndoa na talaka huku wanawake ndio wakiongoza kufungua mashtaka ya masuala ya migogoro ya ndoa.

Aidha ameipongeza Serikali kwa kuandaa kampeni hii ambayo imelenga kuwasaida wananchi kupata haki zao huku akitoa rai kwa wananchi waweze kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ya msaada wa kisheria.

Pia Jaji Khamisi ameeleza kuwa sasa lugha ya kiswahili inatumika mahakamani ili kurahisha mawasiliano na pia ametoa wito kwa Wizara kutengeneza mifumo itakayowezesha wananchi kuwasilisha lalamiko kwa njia ya kielektroniki.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid amesema wanaume nao hunyanyaswa na wanawake hasa katika kuwalazimisha kubadilisha hati za mali zao.

Amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria iwasaidie wananchi wote wanao pitia changamoto hata wanaume kwani kwa muda mrefu wanawake ndio wameonekana wanapitia changamoto nyingi kumbe wapo na wanaume wanaonyanyaswa.

Naye Rais wa Chama Cha Mawakili Zanzibar Joseph Magazi amesema msaada wa kisheria sio anasa bali ni haki ya msingi ya kila mwananchi na kuwa bila mwananchi kupata msaada wa kisheria haki inabaki kwenye makara