Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

MASWI NI KATIBU MKUU BORA KABISA KATI YA NILIOWAHI KUFANYA NAO KAZI- WAZIRI NDUMBARO

Imewekwa: 02 May, 2025
MASWI NI KATIBU MKUU BORA KABISA KATI YA NILIOWAHI KUFANYA NAO KAZI- WAZIRI NDUMBARO

Waziri wa Katiba na Sheria Nchini Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amemtaja Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bwana Eliakimu Chacha Maswi Kama Miongoni mwa Makatibu wake bora kabisa aliowahi kufanya nao kazi serikalini kutokana na kasi, umahiri na mageuzi mbalimbali ambayo amekuwa akiyafanikisha kwa muda mfupi.

"Kwa kipekee napenda Kumpongeza Eliakim Chacha Maswi kwa kuteuliwa kuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na sheria na kwa dhati kabisa naomba nikiri kuwa kupitia utendaji kazi wake mahiri na mzuri, ndugu Maswi amekuwa msaada mkubwa katika kuboresha sekta ya sheria ambapo kwa kipindi kifupi cha takribani miezi tisa tangu ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu amewezesha maboresho mbalimbali kwa Wizara na Taasisi za wizara na hivyo kuchochea ufanisi katika utendaji kazi na kuimarisha upatikanaji haki kwa wananchi." Amesema Dkt. Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro amebainisha hayo wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2025/26 akieleza kuwa Maboresho mbalimbali yaliyofanywa Ndani ya Wizara na Taasisi zake ni matokeo ya imani kubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumuamini na kumpa ridhaa ya kutumika kama Katibu mkuu wa Wizara hiyo.

Waziri Ndumbaro pia amemshukuru Maswi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, akieleza kuwa wamekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha shughuli mbalimbali zenye kutekelezwa na Wizara hiyo muhimu kwa ustawi wa utawala wa sheria nchini Tanzania.