Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

MTANDAO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA JINSIA WAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Imewekwa: 19 Sep, 2025
MTANDAO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA JINSIA WAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi na jinsia Nchini leo Septemba 18, 2025 umejitambulisha rasmi na kuomba ushirikiano baina yao na Wizara ya Katiba na Sheria ili waweze kushiriki kikamilifu katika mapitio na utekelezaji wa sheria mbalimbali zinazolenga masuala ya jinsia na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo Maria Matui ameongoza baadhi ya wajumbe wa mtandao huo walio wakilisha wajumbe zaidi ya 70 na kusema kuwa, “tumeona umuhimu wa Wizara hii inayosimamia sheria zote na kiukweli tumechelewa kuja kujitambulisha ili nasi tuweze kushiriki inapotokea kuna mapitio ya sheria au sera mbalimbali”.

Mtui ameeleza kuwa mtandao huo umekuwa ukitoa elimu kwa jamii kupitia njia mbalimbali kama vile semina, machapisho, marathoni na maandiko mbalimbali ili kuiwezesha jamii kuwa na uelewa juu ya mabadiliko ya tabia yan chi na jinsia.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi amesema Wizara hiyo iko tayari kushirikiana na mtandao huo kwakuwa umelenga kutoa huduma kwa wananchi na hivyo wanaunga mkono juhudi na kazi ambazo wamekuwa wakizitekeleza.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt Franklin Rwezimula amesema jitihada za mtandao huo za kuwafikishia elimu wananchi zinapaswa kuungwa mkono huku akiwaeleza kuwa wanapotoa elimu ya jinsia wasijikite katika jinsia moja bali wazingatie usawa kwa wote kwakuwa mabadiliko ya tabia nchi hayachagui.

Wajumbe wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi na jinsia wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi (katikati) mara baada ya kujitambulisha rasmi na kuomba ushirikiano baina yao na Wizara.