Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Serikali Kuendelea Kusimamia Haki za Watoto – Dkt. Chana

Imewekwa: 05 Jun, 2024
Serikali Kuendelea Kusimamia Haki za Watoto – Dkt. Chana

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 05, 2024 jijini Dar es Salaam amefungua mdahalo kuhusu Sera za ajira kwa watoto uliolenga kuimarisha  ulinzi wa watoto katika kuelekea kukomesha utumikishwaji  wa Watoto Tanzania.

Akizungumza katika mdahalo huo Mhe. Chana amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia haki za watoto na hatua kali zitachukuliwa kwa wote wanaokiuka sheria inayomlinda mtoto.

Chana ameongeza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kumlinda mtoto kwa nafasi yake.

"Wajibu wetu kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha mtoto analindwa, Wazazi nyumbani, Viongozi wa Dini, Walimu mashuleni na jamii kwa ujumla tushirikiane na Serikali tuhakikishe mtoto analindwa." Alisema.

Mdahalo huo unalenga kujadili uboreshaji wa Sera na Sheria mbalimbali zinazomlinda mtoto kukomesha utumikishwaji wa watoto kwenye ajira na kuelimisha jamii juu ya haki za Watoto.