TIAC YAISHUKURU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA USHIRIKIANO

Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi Tanzania (TIAC) wameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kudumisha ushirikiano na Kituo hicho katika kuendeleza na kudumisha matumizi ya Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala
Pongezi hizo zimetolewa wakati ujumbe kutoka TIAC ulipotembelea na kufanya kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi kilichofanyika katika ofisi za Wizara Mtumba tarehe 14 Agosti, 2025.
Ujumbe kutoka TIAC uliongozwa na Bw. Boniphace Mwabukusi rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw. Mpale Mpoki Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TIAC na Bi. Magreth Magoma Afisa Mtendaji Mkuu wa TIAC.
Aidha, katika kikao hicho Wizara na TIAC wamekubaliana kuendeleza ushirikiano katika kukuza matumizi ya Njia Mbadala ya utatuzi wa migogoro ambayo ni njia inayotumia muda mfupi, gharama nafuu na kuimarisha mahusiano katika jamii.