Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

USHIRIKIANO WIZARA YA SHERIA BARA NA ZANZIBAR, KUENDELEA KUNUFAISHA WANANCHI - NW SAGINI

Imewekwa: 05 May, 2025
USHIRIKIANO WIZARA YA SHERIA  BARA NA ZANZIBAR, KUENDELEA KUNUFAISHA WANANCHI - NW SAGINI

Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria (Bara) Jumanne Sagini amesema ushirikiano kati ya Wizara upande wa Bara na Zanzibar umewezesha Kampeni ya Msaada wa Kisheria kuwa na mafanikio makubwa.

Sagini amesema ushirikiano huo ulianza tangu kuandaliwa kwa mkakati wa utekelezaji wa kampeni hadi katika utekelezaji wa kampeni hiyo na sasa umeleta matunda ambayo ni kampeni ya Msaada wa Kisheria kuwa mafanikio makubwa Tanzania bara na Zanzibar.

Ameongeza kuwa kupitia Kampeni hiyo wameweza kubadilisha uzoefu baina ya taasisi mbalimbali za Tanzania bara na Zanzibar kama vile Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ameongeza kuwa ushirikiano huo utakuwa endelevu.