Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WAZIRI NDUMBARO ASIFU UMAHIRI SERIKALI YA AWAMU YA SITA CHINI YA RAIS SAMIA.

Imewekwa: 02 May, 2025
WAZIRI NDUMBARO ASIFU UMAHIRI SERIKALI YA AWAMU YA SITA CHINI YA RAIS SAMIA.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri na uchapakazi wake, uliosababisha mafanikio mbalimbali katika sekta tofauti ikiwemo kwenye sekta ya Sheria nchini kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Wakati akitoa salamu mbalimbali, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba kwa mwaka 2025/26,leo Jumatano Aprili 30, 2025 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri Ndumbaro amempongeza pia Rais Samia kwa kuteuliwa na kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa Mgombea Urais 2025 akiambatana na Mgombea wake mwenza,Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye kwasasa ni Katibu Mkuu wa Chama Chs Mapinduzi.

Dkt. Ndumbaro kadhalika ametoa Shukrani kwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko, akiwashukuru kwa Uongozi wao na ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiutoa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wizara hiyo ya Katiba na Sheria nchini.