Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WAZIRI NDUMBARO KUHUDUMIA WANANCHI SABASABA IJUMAA JULAI 11, 2025

Imewekwa: 10 Jul, 2025
WAZIRI NDUMBARO KUHUDUMIA WANANCHI SABASABA IJUMAA JULAI 11, 2025

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro, anatarajiwa kuwahudumia wananchi kwa kutoa Huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za msaada wa Kisheria bure katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2025) siku ya Ijumaa Julai 11, 2025.

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Kutoa Taarifa za Haki za Binadamu Bi. Beatrice Mpembo ametoa taarifa hiyo mapema leo Julai 8, 2025 na kuongeza kuwa Waziri Dkt. Ndumbaro atapokea na kushughulikia migogoro ya ardhi, ndoa, miradhi, ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia na watoto, jinai na Madai.

“Kesho Mhe Waziri Dkt. Ndumbaro atakuwepo yeye mwenyewe na atawahudumia wananchi watakaofika katika banda letu, hivyo tunawakaribisha wananchi wote waje kwa wingi walete malalamiko na changamoto zinazo wakabili pia watapata elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria atakayoitoa”, amesema Mpembo.

Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi katika maonesho ya Sabasaba hadi tarehe 13 Julai 2025 kupitia Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Katiba na Ufuatiliaji Haki, Haki za Binadamu, Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri wa asili na Maliasilia za Nchi pamoja na Huduma za Msada wa Kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.