Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAIKABIDHI TLS VIFAA VYA TEHAMA

Imewekwa: 18 Sep, 2025
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAIKABIDHI TLS VIFAA VYA TEHAMA

Wizara ya Katiba na Sheria Septemba 16, 2025 imekikabidhi Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) vifaa vya Tehama (server) vyenye uwezo mkubwa wa kutunza taarifa mbalimbali ili kuendeleza matumizi ya Tehama katika utendaji wa kazi zao.

Akikabidhi vifaa hivyo katika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi amesema nia ya Serikali ni kuiwezesha TLS kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TLS Mariam Otham ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitawezesha kuongeza ufanisi wa matumizi ya Tehama hususani katika kutunza taarifa za mifumo mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Omary Gabriel amesema vifaa hivyo vitawezesha Wizara kuunganisha baadhi ya Mifumo yake na mifumo ya TLS ili kurahisisha utoaji wa huduma za kisheria kwa wananchi na pia vifaa hivyo vya kisasa vina uwezo mkubwa wa kutunza taarifa nyingi.