Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Jumanne Sagini akizungumza na Mawakili wa Serikali (hawapo pichani) katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya uendeshaji wa mashauri ya Serikali Mei 20, 2024 katika ukumbi wa Lush Garden jijini Arusha.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya Mawakili wa Serikali Jijini Arusha ambapo amesema mafunzo hayo yatahusisha pia tathmini ya namna Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali zimefanikisha kuratibu na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi nje na ndani ya nchi.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uendeshaji wa mashauri ya Serikali yanayofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Mei 20-22, 2024 Lush garden jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akiongoza zoezi la uzinduzi wa nembo ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Kulia kwa Naibu Waziri ni Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, akifuatiwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (aliyeketi katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali kutoka Wizara mbalimbali mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali Mei 20, 2024 Lush Garden jijini Arusha.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiteta jambo na Wakili wa Serikali na Afisa Bunge Aveline Ombock (kushoto) na Wakili wa Serikali Elia Athanas (kulia), Mei 20, 2024 Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati akifungua Warsha ya Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai, Wakuu wa Idara za Mipango na Tathmini na Ufuatiliaji (M&E) katika Taasisi za Haki Jinai, Mei 20, 2024 Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati akifungua Warsha ya Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai, Wakuu wa Idara za Mipango na Tathmini na Ufuatiliaji (M&E) katika Taasisi za Haki Jinai, Mei 20, 2024 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi walioshiriki Warsha ya Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai, Wakuu wa Idara za Mipango na Tathmini na Ufuatiliaji (M&E) katika Taasisi za Haki Jinai, Mei 20, 2024 Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati), Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande (kushoto), Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Warioba (kulia) kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi walioshiriki Warsha ya Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai, Mei 20, 2024 Jijini Dodoma.