Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akisoma hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 29, 2024 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwasili Bungeni, mkononi ameshika mkoba uliobeba Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 29, 2024.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo (kushoto) akiteta jambo na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole, wengine katika picha ni Dkt. Boniphace Luhende Wakili Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mtaafu Mhe. Mathew Mwaimu wakati wakisubiri kusomwa kwa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 29, 2024.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kupitia maeneo ambayo yanahitaji ufafanuzi kwenye bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25. Kikao hicho kimefanyika tarehe 28 Aprili, 2024 ofisi za Wizara Mtumba. Bajeti ya Wizara itasomwa Bungeni tarehe 29 Aprili, 2024.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kupitia maeneo ambayo yanahitaji ufafanuzi kwenye bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25. Kushoto kwake ni Bw. Frank Kanyusi Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa RITA. Aprili 28, 2024 ofisi za Wizara Mtumba.
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience Ntwina (kushoto), Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo – Law School of Tanzania Prof. Sist Mramba (kulia) wakati wa kikao cha kupitia maeneo ambayo yanahitaji ufafanuzi kwenye bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25. Aprili 28, 2024 ofisi za Wizara Mtumba.
Viongozi wengine waliohudhuria kikao cha kupitia maeneo ambayo yanahitaji ufafanuzi kwenye bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25. Aprili 28, 2024 ofisi za Wizara Mtumba.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara kupitia Bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 27, 2024. Hotuba hiyo itasomwa Bungeni Jumatatu tarehe 29 Aprili, 2024.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Mbaraka Stambuli (kulia) wa Wizara ya Katiba na Sheria akitoa wasilisho la Makisio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 27, 2024 ofisi za Wizara Mtumba. Bajeti hiyo itasomwa Bungeni tarehe 29 Aprili, 2024.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa wasilisho la Makisio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 Aprili 27, 2024 ofisi za Wizara Mtumba. Bajeti hiyo itasomwa Bungeni tarehe 29 Aprili, 2024.