''Wizara ya Katiba na Sheria Tunakusikiliza, Tunakuelewa na Tunakusaidia"
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba (Aliyesimama) Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Jana Januari 21, 2026, Bungeni jijini Dodoma.
Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) kikipokea na kujadili taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zilizo chini yake,21 Januari, 2026, Bungeni jijini Dodoma.
Wananchi mkoani Singida wakipata Huduma za Msaada wa Kisheria wakati wa Kliniki ya Huduma za Msaada wa Kisheria iliyofanyika kwa siku mbili mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, Januari, 2026
Wananchi mkoani Singida wakipata Huduma za Msaada wa Kisheria wakati wa Kliniki ya Huduma za Msaada wa Kisheria iliyofanyika kwa siku mbili mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Waziri wa Ktiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, Januari, 2026
Wananchi mkoani Singida wakipata huduma za Msaada wa Kisheria kutoka kwa wataalam wakati wa Kliniki ya Huduma za Msaada wa Kisheria iliyofanyika mkoani humo kwa siku mbili ikiwa ni sehemu ya ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Ndg. Eliakim Chacha Maswi (kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka wakibadilishana Hati za Makubaliano ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa Umma, Januari 8, 2026, Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Ndg. Eliakim Chacha Maswi (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF Bi. Lulu Ng''wanakilala wakisaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa Umma, Januari 8, 2026, Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Chacha Maswi akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF Bi. Lulu Ng''wanakilala baada ya kusaini Makubaliano ya Ushirikiano wa Utekelezaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa Umma, 8 Januari, 2026, Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, akifungua rasmi Kliniki ya Msaada wa Kisheria mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa masuala mbalimbali wakati wa ziara yake ya siku mbili (5 & 6 Januari, 2026 mkoani humo.