• tawla
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akipokea vitabu na vipeperushi mbalimbali vinavyoelezea shughuli zinazofanywa na shirika lisilo la kiserikali la utoaji msaada wa kisheria liitwalo TAWLA kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bibi Tike Mwambipile, Naibu Waziri alipofanya ziara katika shirika hilo.
 • open
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki akiongea na Wahadhiri na Watumishi wa Chuo Kikuu Huria (hawapo pichani) alipokitembelea chuo hicho tarehe 17/7/14 ili kujionea namna shughuli za utoaji msaada wa kisheria zinavyofanyika.
 • HOUSE OF PEACE
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki akipokea mpira wenye ujumbe usemao "usimpige mwanamke piga mpira" kutoka kwa Mwanasheria wa shirika lisilo la Kiserikali la utoaji msaada wa kisheria liitwalo House of Peace alipotembelea shirika hilo tarehe 17/07/2014.
 • cwca
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la utoaji msaada wa kisheria liitwalo CWCA Bibi Utti Mwang'amba Naibu Waziri alipotembelea shirika hilo hivi karibuni.
 • ziara nwks
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa chama cha Wanasheria Tanzania (hawapo pichani) katika ziara yake iliyofanyika tarehe 14/07/2014 katika ofisi za chama hicho. Kulia ni mratibu wa utoaji wa huduma za kisheria Tanzania Bw. Daniel Lema na kushoto ni Makamu wa Rais wa chama hicho Bi. Flaviana Charles.
 • ziara nwk
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (mwenye nguo ya njano) akizungumza na uongozi wa Envirocare katika ziara yake iliyofanyika tarehe 14/07/14 ya kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya utoaji wa msaada wa kisheria nchini. Katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo Bi. Loyce Lema.
 • ziara nww
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki akisalimiana na wafanyakazi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania alipotembelea Taasisi hiyo tarehe 14/07/2014 kwa lengo la kuongea na uongozi na wafanyakazi kuhusu masuala ya utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria nchini.
 • Dkt. Migiro
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro akipokea Taarifa juu ya Mapitio ya Mfumo wa Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe Jaji Aloysius Mujulizi Dodoma Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume Bi. Winfrida Korosso.
 • HAFLA KATIBU MKUU
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde akikabidhiwa shada la maua na Bi. Arapha Mahmoud kwa niaba ya watumishi wa Wizara hiyo katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika tarehe 13/08/2014 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo baada ya kumaliza utumishi wa umma.
 • KATIBU MKUU
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utmishi wa umma iliyofanyika tarehe 13/08/2014 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo.
 • UKIMWI
  Bi. Joyce Mlowe Mratibu wa Masuala ya Ukimwi Wizara ya Katiba na Sheria akizungumza na wajumbe wa kamati ya ukimwi(wengine hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kutekeleza masuala ya ukimwi mahala pa kazi katika mafunzo ya ukimwi yaliyofanyika tarehe 20/08/2014 katika ukumbi wa ukumbi wa mikutano wa Wizara.
 • MAHAKAMA
  Muonekano wa ndani wa Mahakama ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School).
 • NGOLE
  Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole akiwaleza waandishi wa habari lengo la uanzishwaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo tarehe 06/09/2014 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.

Habari Mpya

Viongozi

Upo Hapa: Home

Wizara ya Katiba na Sheria ilianzishwa kwa tamko la Rais toleo Na.20 la mwaka 2008. Wizara hii ndiyo mhimili Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Kisheria katika nchi. Jukumu la msingi la Wizara ni kuhakikisha kuwa kuna utawala wa Sheria unaozingatia Katiba ya nchi.

Aidha, ni jukumu la Wizara, kuona kwamba Serikali na Taasisi zake zinasimamia Sheria kwa ufanisi na kwa dhati na kuwa wananchi wanapaswa kufuata na kuheshimu Sheria. Kwa ujumla Wizara inalo jukumu la kuhakikisha  kunakuwepo mfumo wa Sheria unaotoa fursa sawa kwa watu wote katika jamii ili kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.

 

dhamira
dira
dhamira
dira