Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara kupitia Bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 27, 2024. Hotuba hiyo itasomwa Bungeni Jumatatu tarehe 29 Aprili, 2024.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Mbaraka Stambuli (kulia) wa Wizara ya Katiba na Sheria akitoa wasilisho la Makisio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 Aprili 27, 2024 ofisi za Wizara Mtumba. Bajeti hiyo itasomwa Bungeni tarehe 29 Aprili, 2024.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa wasilisho la Makisio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 Aprili 27, 2024 ofisi za Wizara Mtumba. Bajeti hiyo itasomwa Bungeni tarehe 29 Aprili, 2024.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa wasilisho la Makisio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 Aprili 27, 2024 ofisi za Wizara Mtumba. Bajeti hiyo itasomwa Bungeni tarehe 29 Aprili, 2024.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akiwasilisha Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2024/25 Bungeni, Aprili 25, 2024 Bungeni Dodoma.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (katikati), kulia kwake ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Hamis kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaotokea Wilaya ya Butiama ambao walikuwa wageni wa Mhe. Sagini. Aprili 24, 2024 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Shigeki Komatsubara Aprili 23, 2024 Ofisi za Wizara Mtumba.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Shigeki Komatsubara Aprili 23, 2024 Ofisi za Wizara Mtumba.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati), kulia kwake ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini, kushoto kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Shigeki Komatsubara, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu (kulia) kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki kikao hicho, Aprili 23, 2024 Ofisi za Wizara Mtumba.
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Ndg. Frank Kanyusi Frank akitoa neno la utangulizi kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kabla ya kumkaribisha Kaimu Meneja wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini Bw. Ernest Mbuna kuwasilisha Taarifa ya majukumu ya RITA, Aprili 23, 2024 ofisi za Wizara Mtumba.