Baadhi ya Wananchi wilaya ya Magharibi B, wakifuatilia elimu kuhusu masuala ya Kisheria wakati wa utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika mkoa wa Mjini Magharibi Kisiwani Unguja tarehe 3 Juni, 2025
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Chacha Maswi amewaagiza madereva wa wizara kuhakikisha wanaendeshe magari kwa umakini mkubwa huku akiwaagiza kuzingatia maadili ya kazi yao na kuwaonya wajiepushe na uzembe Maswi ameyasema hayo June 2, 2025 katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Madereva wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara Ndg.Eliakim Maswi katika kikao kilichofanyika Mtumba, jijini Dodoma
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Bi. Fatma Kalovya (wa kwanza kushoto) akizungumza na Madereva wa Wizara ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) kuhusu kuzingatia uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na uzingatiaji wa Sheria za Barabarani na kuepuka mwendokasi.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Rasilimali Watu Bi.Remida Lulambo
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Bi. Fatma Kalovya (wa kwanza kushoto) akizungumza na Madereva wa Wizara ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) kuhusu kuzingatia uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na uzingatiaji wa Sheria za Barabarani na kuepuka mwendokasi.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Rasilimali Watu Bi.Remida Lulambo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula akiongoza kikao kati ya Wizara, wadau na wamiliki wa makampuni ya michezo ya kubahatisha kuhusu Sheria za michezo hiyo. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini, Dodoma tarehe 27 Mei, 2025
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Msaada wa Kisheria wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Abdulrahman Mshamu akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula kufungua kikao kati ya Wizara na wadau na wamiliki wa makampuni ya michezo ya kubahatisha.Kikao kilifanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini, Dodoma tarehe 27 Mei, 2025
Wadau na wamiliki wa michezo ya kubahatisha nchini wakichangia mada katika kikao kati ya Wizara, wadau na wamiliki wa makampuni ya michezo ya kubahatisha kuhusu Sheria za michezo hiyo.Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini, Dodoma tarehe 27 Mei, 2025
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro alipowasili katika uwanja wa Shule ya Msingi Asanga Jijini mbeya kwa ajili ya kufunga mafunzo kuhusu elimu ya Msaada wa Kisheria kwa viongozi wa Serikali za Mitaa jijini Mbeya tarehe 23 Mei, 2025
Afisa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Modekauye Benedict akitoa maelezo wakati wa utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa wananchi na viongozi zaidi ya 4000 jijini Mbeya tarehe 22 Mei, 2025